MIBARAKA ISIYO NA IDADI
*Umngoje BWANA, uwe Hodari, upige moyo konde, naam, umngoje BWANA.* Zaburi 27:14
📝 Uwe na moyo mkuu, dada yangu. Bado kitambo kidogo, nasi tutamwona Yesu. “Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo,ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo” (Yohana 14:1—3).
📝 Jipe moyo katika Bwana. Ninafurahi katika matarajio angavu ya wakati ujao, na iwe hivyo kwako pia. Hebu tuwe na moyo mkuu, na kumsifu Bwana kwa ajili ya wema wake kwa watoto wa wanadamu.Usitazame upande wenye giza. Kuwa na imani kwa Mungu. Tu mali ya Kristo, na hebu tukumbuke kwamba anatupenda, naye atakuwa msaada wetu na Mungu wetu.
📝 Usiku uliopita nilikuwa macho kwa muda mrefu.
Nilifadhaika na kupata wasiwasi; kwa kuwa nilijua wengine walikuwa wakipitia majaribu na majaribio, nami nilijiuliza ni kwa jinsi gani ningeweza kuwasaidia wamtazame Yesu na kuifariji mioyo yao katika pendo lake. Nilitafakari, ninaweza tu kuushikilia mkono wa Kristo na kuisikia sauti yake, nikiwa macho nimejilaza, nikijiombea, na zaidi sana nikiwaombea wanaopitia katika majaribu na majaribio!
📝 Sikupata usingizi baada ya saa saba. Nilisikitika, kwa sababu nilikuwa na kazi ya kuandika ambayo nilipaswa kuifanya leo, na nikafikiri kwamba nisingeweza kuifanya ikiwa nisingelala. Lakini ilipofika saa nane, niliamka na kuvaa nguo, nikawasha moto, na kabla ya kifungua kinywa nilikuwa nimeandika kurasa nyingi. Nimeandika kurasa nyingi tangu baada ya kifungua kinywa, na sikuhisi kuwa mwenye usingizi kabisa.
📝 Hebu tuwe na shukrani kwa kila hisani. Hebu tujaribu kuwa Wakristo wenye kuangaza. Roho zinazofanya nifadhaike, ninazopata wasiwasi kwamba hazitavumilia hadi mwisho, nitazikabidhi kwa Mungu. Ile iliyo halisi ya kiungu itang’aa katika giza la kimaadili, kwa kuwa nuru ya Kristo huiangazia. Kwake tunawiwa kudumu kumpa sifa na shukrani; kwa kuwa tunatunzwa na nguvu zake kwa imani. Hatuwezi kujihifadhi wenyewe.
🔘 *Jipe moyo. Bwana anakupenda, na kukuhurumia kwa kila udhaifu wako. Kwa hakika atakutia nguvu na kukubariki, ikiwa tu utamtumaini. Moyo wa Mungu asiye na kikomo usingeridhishwa kuwapatia wale wampendao Mwana Wake baraka kidogo kuliko anavyompatia mwana wake.*
*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮♂️
No comments: